Kombe la Mapinduzi lafunguliwa rasmi leo laaza na kundi ‘B’

Pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi linafunguliwa rasmi leo kwa kuchezwa mchezo mmoja baina ya Malindi dhidi ya KVZ wote kutoka Kundi B mchezo huo utachezwa majira ya saa 10 za jioni.

Michezo mingine itandelea kuchezwa Jumatano Chupkizi dhidi ya Mlandege majira ya saa kumi za Jioni wakati majira ya usiku Jamuhuri atacheza dhidi ya Azam Fc mabingwa watetezi wa mashindano hayo.

Vinara wa Ligi kuu ya Zanzibar kwa sasa Kvz watacheza dhidi ya Yanga January 3 majira ya saa 2 za usiku huku Simba wakiwa na mchezo wao dhidi ya Kmkm kwenye mzunguko wa kwanza wa mashindano hayo.

Wakati maandalizi mbali mbali yakiendelea kwenye mashindano hayo ya Mapinduzi Cup kusherekea kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari taa za uwanja wa Amani na marekibisho ya ubao wa kusoma matokeo umesharekebishwa.

Kombe la Mapinduzi limeunda makundi mawili Kundi A Chupkizi, Mlandege,KMKM na Simba na upande wa undi B Malindi, Kvz, Jamuhuri Azam na Yanga.