Kuelekea uchaguzi mkuu Uganda ambao unatarajiwa kufanyika Januari 14 Serikali ya nchi hio imetoa maagizo kwa Watoa huduma za Internet kuzima Mitandao yote ya kijamii na App nyingine zinazotumika kutumiana msg, maamuzi haya yametolewa zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kura kupigwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Alhamisi.

Watumiaji wa Mitandao Uganda walianza kulalamika kuanzia jana Jumatatu January 11 kuwa wanashindwa kutumia Facebook, WhatsApp na Mitandao mingine.

Taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Uganda imesomeka “ Tunakuagiza haraka iwezekanavyo zima Mitandao yote ya kijamii na App hadi itakapoamriwa vinginevyo”