Kulikoni Haji Manara na zawadi hii kwa Diamond Platnumz
Afisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amemkabidhi tuzo msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz kwa niaba ya klabu yake ya Simba.
Manara amemkabidhi Diamond tuzo hiyo kwenye siku yake ya kuzaliwa hapo jana siku ya Jumanne mbali na zawadi hiyo amempatia keki yenye nembo ya Simba kutokana na msanii huyo kuwa shabiki mkubwa wa klabu hiyo.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Manara amemwagia sifa msanii huyo kuwa ni mwanamuziki mkubwa ulimwenguni.