Wanamgambo wa Alshaabab nchini Somalia wamekiri kuhusika na shambulio lilotokea katika hoteli ya kifahari mjini Mogadishu SYL nchini humo. Taarifa zinasema kuwa makundi ya wanajeshi wanaonekana kwenye barabara inayoelekea katika kasri ya Rais.

Kituo cha redio cha Dalsalam mjini Mogadishu kimesema kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa wabunge wawili kwa jina Mahgan pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Somalia Abdulkadir Ali Omar wamejeruhiwa katika shambulio lilitokea katika hoteli ya SYL.

Msemaji wa Serikali, Ismail Mukhtar kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, Watu 10 wameuawa katika shambulio hilo ambapo Wanamgambo wa Al Shabaab watano waliovamia hoteli hiyo wameuawa na Watu wengine watano wakiwemo raia wa kawaida wawili.

Aidha, Watu takriban 82 wameokolewa na wengine wengi wamejeruhiwa huku Polisi ikitahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na shambulio hilo katika hoteli hiyo iliyopo karibu na makazi ya Rais na inayotumiwa zaidi na Viongozi Waandamizi wa Serikali.