Kusaga afunguka juu ya tetesi zinazosambaa mitandaoni

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amejibu tetesi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumiliki vituo viwili vya runinga na radio, Wasafi TV na Wasafi FM.

Kusaga akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 amesema kuwa yeye anamiliki karibia vituo vyote vya radio za vijana hapa Tanzania.

Hapana mimi sitakwenda huko, mimi  namiliki radio zote za vijana, radio zote za vijana mimi namiliki, kwa njia moja au nyingine, ukimuita Seba atakwambia umenielewa. Lakini labda ni kwa sababu ya kuongeza wigo, labda wigo wetu sisi unaweza ukawa hautoshi, mimi nashiriki kwenye industry yote ya burudani”

Kwa upande mwingine, Kusaga amesema kuwa anashirikiana na radio nyingine za mikoani kama Safari FM ya Mtwara na Jembe FM ya Mwanza.

Awali kabla ya kutoa tamko hilo, kulikuwa na tetesi kuwa Joseph Kusaga  ndiye mmiliki wa vituo vya Wasafi TV na Wasafi FM .