Kusaga azungumzia kuhusu mshahara wa Milard

Mkurugenzi na bosi wa Clouds Media Group Joseph amefunguka kuwa Milard alianza kufanya kazi na kulipwa mshahara na wao lakini kwa sasa mshahara wa Milaard ni mkubwa kuliko hata wa kwake lakini kwake hiyo ni sifa kwa sababu mwisho wa siku wanataka kuwafanya vijana kuwa imara na kile wanachokifanya.

Kusaga amefunguka na kusema kuwa katika watu anaojivunia nao ni millard ayo ambae alianza kufanya kazi Clouds Medai Group na mpaka sasa amekuwa akifanya kazi kubwa zaidi.

Amebainisha hayo katika maswali aliyokuwa akiulizwa siku ya jana ambapo clouds media ilikuwa itimiza miaka 19 tangu kuanziswa kwake, Joseph kusaga anasema hawezi kumuonea wivu wala kukataa mafanikio ya milaard ayo kwa sababu amekuwa moja ya vijana waliojituma sana kufika walipo.

Hata siku za nyuma Milard alipowahi kuulizwa kuhusu kufungua radio yake kwa sababu kwa sasa anaweza kusimama mwenyewe alisema kuwa bado ana deni kuwa sana ndani ya clouds media hawezi kuacha kazi hapo.