Ikiwa Leo July Mosi Ligi kuu Zanzibar inatarajiwa kuanza kuchezwa katika Vituo viwili tofauti vya Unguja na Pemba.

Ambapo mchezo wa mwanzo wa Ligi kuu Zanzibar unatarajia kuanza majira ya Saa 8:00 Selem View wataikaribisha Mafunzo katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limefuta kadi zote za adhabu kwa wachezaji waliooneshwa wakati ligi kuu ilipochezwa awali na sasa kuanzia Leo watacheza wakiwa safi isipokua mchezaji/wachezaji ambao watapata kadi zitaanza kuhesabiwa tena upya.