Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF)  limebadilisha ratiba yake ya kuanza kwa ligi kuu Zanzibar ya msimu wa 20/21.

ligi kuu Zanzibar ilikua inatarajiwa kuanza Novemba 7 mwaka huu kwa msimu wa 20/21 na sasa ligi hiyo itachezwa kuanzia Novemba 14 na ngao ya jamii itachezwa Novemba 8.

Sababu kubwa ya ligi hio kusogezwa mbele ni kupisha uchaguzi mkuu wa nchi.