Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  amesema  mgogoro uliopo ndani ya chama chao ni figisu figisu inayotokana na Mh Lipumba pamoja na msajili wa vyama vya siasa Jaji Fransic Mutungi.

maalim Seif ameyasema hayo leo katika kipindi cha Clouds360 kinachorushwa na  Clouds TV na kuwataka wananchi kufahamu kuwa chama hicho hakitavurugika daima.

Maalim pia aliwataka wanachi kufahamu kuwa hakuna CUF ya maalim Seif wala CUF ya Lipumba bali chombo kikuu cha CUF ni mkutano mkuu ambao ndio unaotoa maamuzi ya chama.

kwa upande walipumba maalim Seif alisema kuwa chama hakikumfukuza uanachama bali kilimshauri  na kumtumia watu mbali mbali kumshauri asindoke lakinin aliamua kwa makusudi kujiuzulu na sasa si mwanachama tena wa chama cha CUF.

Akizungumzia uchguzi wa mwaka 2015 Amesema “takwimu zilionesha kuwa nimeshinda lakini sikutangazwa pia Jecha alifanya ubepari wa kufuta uchaguzi bila kushirikisha wenzake wakati hata katiba ya Zanzibar haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi”.