Mgombea Urais waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa uhaba wa watu kweye mikutano yake na wingi wa watu kwenye mikutano ya wagombea wengine wa Urais haumtishi kwani hio sio dalili ya ushindi.

“Mimi nakwenda Vijijini ambako kuna changamoto kubwa za wananchi na sio kukusanya watu kwenye malori na mabasi kuwapeleka kwenye mikutano”

“Kampeni mpaka hivi sasa zinaendelea vizuri na nimejikita zaidi kwenda Vijijini maana ndiko ziliko kero za Watanzania, mimi siishii Mijini kama wenzangu ambao wamekuwa wakikusanya watu” amesema Lipumba.