Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, amesema amesitishiwa mshahara na posho za kibunge tangu Januari 2019 bila kuelezwa sababu zozote za hatua hiyo na kusema anakusudia kuchukua hatua za kisheria kufikisha suala hilo.

Lissu amemtaka Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai na Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai kurejesha mshahara wake na stahiki zake za kibunge.

Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ametoa malalamiko Jumatano Machi 13, 2019 kupitia waraka uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ukizungumzia jinsi anavyonyimwa stahiki zake za msingi akiwa mbunge.