Maagizo 13 kwa Mawaziri Zanzibar


1. Kila waziri aijue wizara na Taasisi zake kwa kuzitembelea.

2. Watengeneze Mpango kazi na Bajeti kwa kutumia ilani, hotuba ya Raisi, ahadi za kampeni, Wapate maoni ya Wadau wa wizara, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar

3. Tembelea miradi yote ya wizara kwa kuangalia ubora, utaratibu wa zabuni, malipo yaliyofanyika, muda wa kumaliza.

4. Uwajibikaji wa Watendaji. Kila mtu awajibike kwa kazi aliyopewa. Huduma zitolewe inavyotakiwa. 

5. Hakikisheni haki za watu zinatolewa. Wafanyakai walipwe Posho zao fedha za safari overtime walipwe.Haki za wananchi zitolewe. Watu wasikilizwe. Oridha ya ardhi zikizotolewa kipindi cha kamapeni za uchaguzi.

6. Utawala bora. Rushwa ubadhirifu uondolewe. Wizi wa makusanyo, frdha za bajeti kuibiwa. Fedha za miradi zinatumika vibaya.

7. Ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Maduhuki hayakusanywi. ZRB na TRA ziangaliwe. 

8. Ubunifu Kila mtu abuni mambo mapya katika kazi. Usisubiri uelekezwe. Tumia wataalamu waliopo kuleta ubunifu.

9. Urasimu: ondoweni usimbufu katika kupata huduma. Njoo kesho njoo kesho iondoke. Wananchi wapate majibu. Mambo yenye maslahi ya Umma yasicheleweshwe. 

10. Muwe wepesi wa kuleta mapendekezo ya sheria pale ambapo sheria ni kikwazo.

11. Utoajibwa taarifa zinazofanywa kwenye vyombo vya habari. Kuweni marafiki wa vyombo vya habari.

12. Sikilizeni malalamiko ya watu. Kila wizara iwe na utaratibubwa kusikiliza malalamiko ya watu. Tumieni teknolojia kutekeleza hili. 

13. UsafiWizara na ofisi baadhi ni chafu. Ofisi zisiwe stoo. Maeneo ya kazi yawe safi.

Miji ni michafu haina hadhi. Itafutwe njia mbadala ya kubafilisha hali hii. Nitakuja kwenye kila Wizara kupata maelezo. Ninewateua na nina matumaini nanyi. Nendeni ofisini mkafanye kazi. Yaliyopo nje ya uwezo naa malaka yenu  yaleteni kwangu.