Kamisheni ya Afya ya Taifa la China imesema, kasi ya maambukizi ya Kirusi Corona inaelezwa inaweza kuongezeka sana na kuna uwezekano idadi ya wagonjwa ikaongezeka pia

Mpaka sasa watu zaidi ya 2,000 wameshaambukizwa Duniani na watu 56 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo

Kirusi hiki, kinaaminika kilianza katika Soko la Bidhaa za Baharini mwishoni mwaka 2019, katikati ya Jiji la Wuhan, China ambalo lilikuwa linauza Nyama ya Porini

Kirusi hiki kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, na Canada

Jana Jumapili, China ilitangaza Katazo la Kuuza Nyama ya Porini katika masoko, migahawa na mitandao ya kieletroniki ya biashara nchini kote