Maamuzi ya RC Makonda kutekwa Mo Dewij

Tutapita katika mahoteli ya Dar Es Salaam kukagua taarifa za miezi mitatu nyuma kujua kuwa wageni wenu waliokuwa wanakuja wanafanya shughuli gani.

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ametoa tamko hilo linalohusu wamiliki wa Mahoteli katika jiji la Dar Es Salaam kufuatia tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara mkubwa dunia Mo Dewij.

Mfanyabiashara maarufu Tanzania Mo Dewji ametekwa na watu wasiojulikana

Makonda ameyasema hayo akiwa eneo la tukio katika hoteli ya colosseum iliyopo Masaki jijini Dar es salaam ambako ndio alikuwa anaelekea kwa ajili ya mazoezi alfajiri kabla ya kukumbwa na tukio hilo.

Kauli ya baba mzazi kutekwa kwa Mo Dewji

“Wenye mahoteli wote kama tuna pata wageni na wageni wanafanya matukio yote haya maana yake hoteli zetu zinawekwa sehemu ambako watu wanatumia, kwahiyo mahoteli yote tutapita kukagua taarifa za miezi mitatu nyuma kujua kuwa wageni wenu waliokuwa wanakuja wanafanya shughuli gani”