Madereva na Wananchi wamelalamikia baraza la Manispaa la Mjini kutokuwa tilia kifusi eneo la kituo cha haile -salasi kutokana kwa kuwepo kwa shimo la maji pamoja na uchafu wataka taka.

Wakizungumza Zanzibr24 huko Kituo cha haile salasi wamesema kuwa wanalipa pesa zao kila siku shilingi 1000 lakini hawaoni ubora wowote katika eneo hilo na kuwataka kufanyia usafi eneo hilo pamoja na uwekaji wa kifusi katika shimo hilo ilikuondoa usumbufu kwa madereva na wananchi wanaofika eneo hilo kwa ajili ya huduma za daladala.

Nae Msaidizi Afisa wa Uhusiano Hassan Yahya Hassan amesema kuwa vituo hivyo bado havijawa rasmi wakati serekali iko katika mchakato wakutenga eneo lililorasmi ili kuimarisha nyundo mbinu hiyo kwa watumiaji ikiwemo kituo cha daladala cha Kijangwani .

Sambamba na hayo Hassan amewaomba madereva na wananchi waendelee kutumia maeneo hayo kwa sasa hadi pale pakionekana kuna hitaji ya kuboresha maeneo hayo kwa njia ya kuweka kifusi ili Daladalaa hizo zitoe huduma bila Ya usumbufu

Rauhiya Mussa Shaaban