Ikiwa Dunia inajiandaa kuupokea mwaka mpya 2019 ifikapo majira ya saa sita kamili za usiku wa leo, Waislamu kote nchini wametakiwa kuitumia siku hiyo kufikiri khatma ya maisha yao na si kusherehekea kama wanavyofanya wengine.

Kikawaida unapoingia mwaka mpya watu husherehekea kwa njia tofauti wengi wao hujichanganya katika kumbi za starehe baadhi hulewa na kuvunja chupa barabarani jambo ambalo limepingwa vikali kufanywa na waumini wa Dini ya kiislamu.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya Ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) Sheikh Khamiss Yussuf Khamiss wakati akizungumza na Zanzibar24 amesema Siku zilizoamrishwa kisharia kusherehekewa na Waislamu ni mbili tu nazo ni sikukuu ya Eid L-Fitri na Eid L-Hajj hivyo kinyume na siku hizo Muislamu hatakiwi kusherehekea

Amesema mambo matatu anayotakiwa kuyafanya Muislamu unapofika mwaka mpya ni kumshukuru Mungu, kuzingatia aliyopitia katika mwaka uliopita na kujiandaa na Umauti.