Chama cha mapinduzi CCM kimevuna madiwani watano wa Chama cha ACT-Wazalendo manispaa ya Kigoma Ujiji.

Madiwani hao wametangaza kujiuzulu na kujiunga na CCM katika ofisi ndogo za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam . mbele ya katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho tawala nchini Tanzania, Humphrey Polepole.

Madiwani hao ni Hamis Rashid (Gungu), Abduli Nasoro (Kasingirima), Foard Sefu (Kasimbu), Ismael Husen (Kagera) na Mussa Ngongolwa (Kipampa).