Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Waislam ya Canberra, yanayopinga uwepo wa vituo vilivyopo nje ya Australia vya kuhifadhi wahamiaji katika visiwa vya Nauru na Manus ambapo mamia ya wakimbizi wanaotaka kuingia nchini humo wamekuwa wakipelekwa huko tokea mwaka 2013.

Diana Abdel Rahman, Rais wa shirika lisilo la kiserikali la Australian Muslim Voice amesema huduma wanayopata wakimbizi katika kambi hizo ni mbaya kuliko wanayopewa wanyama.

Maafisa wa serikali wamesema kwa sasa kuna takribani wakimbizi na waomba hifadhi 915 katika visiwa vya Nauru na Manus.