Serikali yatoa tamko kupanda kwa bei ya Mafuta Zanzibar

Wizara ya Ardhi , Nyumba ,Maji na Nishati imesema Tatizo la kupanda kwa bei za Mafuta Zanzibar linasababishwa na kupanda kwa bei hizo katika soko la Dunia

Akiuliza swali la Msingi katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Paje Jaku Hashim Ayoub alietaka kujua Serikali ina Mpango gani wa Kuingiza mafuta kwa bei nafuu.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Juma Makungu Juma amesema ni kweli bei za mafuta zinashuka na kupanda kutoka na mabadiliko ya bei kutoka katika soko la dunia.

Amesema mafuta yanayotumika Zanzibar huagizwa na makampuni manne ambayo kabla ya kufikishwa Zanzibar Mafuta hayo huhifadhiwa katika Bohari ya Dar es salam na Bandari ya Mombasa ambapo makampuni hayo hulazimika kulipa kodi na kupelekea bei ya mafuta kupanda.

Aidha amesema tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi baada ya kujengwa miundombinu ya mafuta ikiwemo Bandari na Matangi itakayowezesha meli kubwa za mafuta kuja moja kwa moja kwa ajili ya kushusha mafuta jambo ambalo litasaidia kuondoa tatizo hilo Nchini.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.

fathiyashehe@gmail.com