Mahakama Kuu imemrudishia kibali kwa muda kuhudhuria mikutano ya Ikulu ya Marekani Mwandishi wa habari wa CNN aliyezuiwa na Rais Trump, Jim Acosta

Shirika la habari la CNN liliishtaki Ikulu kutaka kurudishiwa kibali kwa Acosta baada ya kutokea mkwaruzo mkubwa kati yake na Rasi Trump hivi karibuni.

Leo Ijumaa, Jaji Timothy Kelly ameamuru Mwandishi huyo kurudishiwa vibali vyake na kuendelea na kazi zake za kuhudhuria mikutano Ikulu kwa muda wakati kesi ikiendelea.

Siku mbili zilizopita Rais Trump na Mwanahabari huyo walizozana katika mkutano wa Trump na Wanahabari baada ya kuulizwa kuhusu siasa zake na Urusi kuingilia chaguzi za Marekani mwaka 2016.