Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali Shauri la kupinga muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililofunguliwa na wanasiasa.

Waliofungua kesi hiyo ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na Joran Bashange na Salum Bimani wote wa CUF.

“Mahakama imeondoa Shauri letu dhidi ya Serikali kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa na kifungu cha 8(3) cha sheria ya Haki na Wajibu ( BRADEA ) kwa sababu ya maombi hayo 2  kuunganishwa. Kufuatia uamuzi huo wa mahakama tumeagiza mawakili leo wafungue kesi mpya ya BRADEA,” ameeleza Zitto Kabwe baada ya uamuzi huo wa Mahakama.