Kufuatia maelekezo yalotolewa na Serikali machi 17/2020 juu ya kujikinga na kupunguza kuenea kwa virusi vya CORONA Mahakama kuu Zanzibar imesitisha usikilizaji wa kesi zote kwa muda wa siku 30 kuanzia leo machi 26, 2020 hadi April 24, 2020 ili kupunguza mkusanyiko wa watu.

Hayo yameelezwa na mrajisi wa Mahakama Kuu Bw. Mohamed Ali Mohamed wakati akisoma taarifa hio kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Jaji Mkuu Omar Othman Makungu huko ofisini kwao Vuga Mjini Unguja

Amesema “kwa sasa mahakama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana,muombaji na wakili wake au ombi la wadhamini ndio watakaoruhusiwa kuingia mahakamani”

“katika kipindi hichi watendaji wote wa mahakama wataendelea kuwepo kazini na kumbi za mahakama(Open Court) zitatumika kwa majaji na mahakimu wenye hukumu na maamuzi(Ruling) watatumia kipindi hichi katika kuzikamilisha “