Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo ya aliyekuwa Mkuu Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa

Mwaka 2016, Bageni aliwasilisha maombi ya marejeo mahakamani hapo akiiomba mahakama hiyo ibadilishe uamuzi wake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Azam Tv, Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ya Bageni ulioandaliwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliosikiliza maombi hayo, umetolewa jana Jumatano, Agosti 14, 2019 na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu.