Mahakama ya Vileo yashindwa kuzifungia Baa za Wilaya ya Kati Unguja

Mahakama ya Vileo Zanzibar  haikufungia baa hata moja wilaya ya kati na kutoa vibali 17 kwa  wafanyabiashara kuendelea kuuza pombe kwa mwaka huu 2019.

Akitoa maamuzi hayo  katika Mahakama Wilaya ya kati Hakimu Mohamed Subeit amesema ameamua kuziruhusu baa hizo zote 17 baada ya kuridhishwa na uendeshwaji wa biashara hiyo kwenye maeneo hayo. 
Amesema Bodi ya Vileo ilifanya ukaguzi na kuona mandhari ya baa zote za wilaya ya kati kuwa yapo salama  na yanaridhisha. 

Hata hivyo amewataka wafanyabiashara wa pombe kuendelea kufuata Sheri ikiwemo kulipa kodi zote za serikali ili kuchangia pato la taifa na kukuza maendeleo na ajira kwa vijana. 

Kwaupande wake Katibu wa Vileo Saleh Ali Abdalla amesema nje ya Mahaka kuwa Mahakama inaendelea na kazi ya utoaji wa maamuzi ya vibali kwa kwa wilaya mbali ikiwemo Magharib A ,Kusini na kwengine ni kaskazin Unguja. 
Amina Omar.