Mashambulizi ya angani yaliozinduliwa na majeshi ya serikali ya Nigeria yamewaua majambazi 12 wenye silaha katika misitu ya Kamuku katika jimbo la kaskazini la Kaduna, jeshi hilo lilisema Jumatano.

Shuguli za kijeshi Jumanne pia ziliwezesha kuwachiliwa uhuru waathirika 15 waliokolewa, alisema Ibikunle Daramola, msemaji wa Jeshi la Ndege la Nigeria.