Majivu ya mwili wa aliyekuwa Rais wa nchi  Cuba, Fidel Castro yamezikwa mjini Santiago, siku 9 za maombolezo zamalizika rasmi watu waendelea na kazi.

Familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa Cuba, Jose Marti.

Hapo jana rais wa Cuba, Raul Castro alisema serikali yake imekataza barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Fidel mwenyewe alivyoagiza.

wakati wa uhai wake rais huyo ilisema waziwazi kuwa hapendelei kitu chochote katika nchi hiyo kupewa jina lake.