MAKALA: Msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar ni mageuzi makubwa ya mpira

Wakati zimebaki siku chache ligi kuu ya Zanzibar mwaka 2018/2019 zinazo tarajiwa kuanza Otoba 20 imeonekana kuwa wadau wengi wamekuwa na shauku ya kuona mabadiliko ya mpira wa Zanzibar hususan ligi kuu ya Zanzibar.

Wakati zimebaki siku chache pazia la msimu wa ligi kuu ya Zanzibar mwaka 2018/2019 linatarajiwa kuanza Oktoba 20 wadau wengi wamekuwa na hamu kuona mabadiliko ya mpira wa Zanzibar hususan ligi kuu ya Zanzibar ambayo imekuwa kama vile wadau wana kiu kubwa ya kusubiri na kuona tunakwenda kupiga hatua.

Tunakwenda kucheza ligi kuu ya Zanzibar huku tukiamini Viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza japo ni kamati ya mpito lakini tunategemea kuona soka la Zanzibar linakuwa si la kawaida kwa vile namna ratiba ya ligi kuu ya Zanzibar ilvyopangwa ili kutoa fursa kwa wadau kushuhudia michezo ya ligi kuu ya Zanzibar 2018/2019.

Mfumo wa Ligi moja yaani kucheza ligi moja na kuondosha mfumo wa kanda ya Unguja na kanda ya Pemba mfumo huu ulikuwa ukitumika kabla si mfumo mzuri sana kwa vilabu vyetu imetengeneza utabaka yaani Unguja na Upemba kama vile tunakuwa tunacheza ligi tatu kwa mwaka mmoja.

Mfumo mpya wa kucheza Ligi moja umekuja na kupokelewa vizuri sana na wadau wa mpira wa miguu Zanzibar kwa vile mafahari wakubwa kutoka pande zote mbili wanakuja kukutana kwenye ligi moja yenye ushindani si wa kawaida.

Kocha Salum Bausi ni moja ya wachezaji wa zamani waliowahi pia kuifundisha timu ya Taifa ya Zanzibar kwa mafanikio makubwa umezugumzia mfumo huu na kusema hapa ndio wazanzibar wanapopataka kuona tunacheza ligi moja na kuondosha mfumo wa kanda ambao unaweza kutengeneza Bingwa katika manzigira ya kukutanisha.

Baadhi ya wadau nao hawakuwa nyuma kuhusu mfumo huu ligi kuu ya Zanzibar ambao kwa muda mrefu haukuchezwa lakini kwa sasa tunatarajia kuona mabadiliko Dadi Ali Dadi ni moja ya wadau wa mpira wa miguu amesema anategemea sana ushindani hususan kwa vilabu vikongwe kama vile Jamuhuri,Mwenge ambavyo viko tayari kupambana kutoana jasho ili kusogeza mpira wa kisiwani pemba ambao kama vile uko chini kwa muda mrefu.

Suala la udhamini sio mjadala mkubwa sana kwenye ligi ya Zanzibar mipango inahitajika sana kuona ushindani mkubwa utakao fanya vinara wa ligi kuu ya Zanzibar Jku na Zimamoto kupata changamoto kubwa ya ushidani licha ya kuwa miongoni mwa vilabu vinakuwa na nafasi kubwa kufanya vizuri kimataifa.

Mabadiliko ya kanuni moja ya jambo la kupeana moyo sana badala ya timu 4 kushuka daraja msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar kwa sasa jumla ya vilabu sita vinatarajiwa kushuka daraja msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar hivyo ni kazi ya wadau kujitokeza viwanjani kuunga mkono mpira wetu.