MAKALA: wachezaji vinara tukao waona ligi kuu ya Zanzibar msimu huu 2018/2019

Oktoba 20 ndio panzia rasmi la ufuguzi wa ligi kuu ya Zanzibar linafunguliwa huku kiu kubwa kuona nani ataonyesha uhodari ndani ya msimu huu ambao unashangwe na mbwembwe za aina yake baada ya kamati kujipanga vyema kusimamia mpira wa Zanzibar kwa uandilifu bila ya muhali.

Wakati jumla ya vilabu 19 vinakwenda kuonyeshana nguvu msimu huu katika makala hii ya Ligi kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka 2018/2019 tunakwenda kuona wachezaji vinara ambao watakaoonekana ndani ya msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar ambao watakuwa kivutio na hamasa kwa vilabu vyao baada ya kuwa na mchango mkubwa ndani ya Timu zao.

Ibrahim Hamada Hilika, (mshambuliaji) , Simba ambaye msitu wake ni ligi kuu ya Zanzibar mchezaji mwenye kiu ya kufunga goli ,mwenye nguvu akiwa uwanjani unamuona mchango mkubwa ndani ya klabu yake kongwe ya Zimamoto ameonekana kwenye nusu msimu uliopita aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka 2015/2016 kwenye hatua ya nane bora .

Amejiunga kwenye klabu ya Bokavu Congo baada ya kuonyesha kiwango cha juu ndani ya Timu ya Taifa ya Zanzibar Heros kule Kenya kwenye mashindano ya CECAFA aliwahi kuhusishwa na vilabu kama vile Yanga na Simba ila haikuwa  kweli ila huenda msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar akarudi kwenye jeshi lake la Zimamoto na kufanya maajabu makubwa ya kuonyesha uwezo wake.

 

Kassim Suleiman Khamisi (Mshambuliaji), Moja ya shauku kubwa kwa klabu ya Jangombe boys msimu huu baada ya kumsajili mshambuliaji huyu aliechwa kwenye klabu yake ya Tanzania Prisons ya Mbeya jina lake kubwa kwa Tanzania huenda tukaona hatari ya mshambuliaji huyu nyota wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heros baada ya kufunga magoli asali kwenye michuano ya CECAFA dhidi ya Rwanda na Tanzania bara na kuwa majeruhi kwa muda mrefu ila kwa sasa amerudi tena kwenye ulingo wa Ligi kuu ya Zanzibar aliwahai kuitumikia klabu yake ya Chwaka saivi imepotea kwenye ligi kuu ya Zanzibar na kurudi ligi kuu ya Zanzibar sasa atampambana na kina Ibrahim Hilika.

 

Mwalim Muhamed (Mshambuliaji), kule kisiwani Pemba anaitwa Teacher yaani mwalimu kunzia jina paka fani yake aliyoisomea ni mshambuliaji wa klabu ya Jamuhuri moja ya washambuliaji mahiri sana ndani ya Jamuhuri kwa uzoefu wake mkubwa wa kufamani nyavu kwenye ligi kuu ya Zanzibar aliwahi kuwa mshambuliaji mzuri kisiwani pemba kwenye hatua za kanda ya ligi kuu ya Zanzibar pia kwenye kumbu kumbu ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi ilomaliza aliwahi kufunga goli la pekee dhidi ya URA ya Uganda na kuifanya Jamuhuri kuifunga timu ngumu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania .

Tunategemea atakuwa ni chachu ndani ya klabu yake ya Jamuhuri msimu huu na kufanya makubwa ili kuletea sifa klabu yake ya Jamuhuri.

Khamisi Mussa Makame (Raisi)( Mshambuliaji), moja ya jina kubwa sana kwenye ligi kuu ya Zanzibar Khamisi Mussa tunamwita ‘’Lack Man’’ mtu mwenye bahati anapokuwa uwanjani huitendea haki nafasi ya ushambuliaji .

Amejiunga na klabu ya Malindi badala ya kutoka Jangombe boys ni mstaarabu lakini anajuwa sana mpira fundi wa kufunga yaani ‘’Finishing striker’’ anarekodi nzuri kwenye ligi kuu ya Zanzibar kama vile Ibrahim Hilika baada ya kufunga magoli mengi ndani ya ligi kuu ya Zanzibar.

Khamisi Raisi pia anarekodi nzuri ya kuifungia klabu yake ya zamani ya Jangombe Boys magoli mawili kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ya mwaka 2016 dhidi ya URA ya Uganda na kuifanya Jangombe Boys ndio timu ya kwanza kuifunga URA kwa Zanzibar kabla ya Taifa jangombe na Jamuhuri, pia Khamisi ana rekodi ya kushinda magoli mawili fainali ya Zanzibar Heros dhidi ya Kenya hivyo ni wazi tunakwenda kuona ushindani wa ndani ya msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar.

Nassor Matar (Mshambuliaji), moja ya washambuliaji wenye kasi ndani ya Klabu ya Jku ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar ni mchezaji kiumbo kama vile mzito lakini anajivunia kuwa ni mwenye nguvu na kasi ya ushambuliaji wa aina yake.

Anarekodi nzuri kwenye ligi kuu ya Zanzibar kwa kufunga magoli ya mbali ya mashuti pia anarekodi ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya KAGAME CUP yalomalizika hivi karibuni ndani ya klabu yake ya Jku na kuwafanya Jku kuwa ndio timu iliofanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Abrahman Chinga (Mshambuliaji) , moja ya washambuliaji wa zamani wa klabu ya Jangombe Boys alifanya vizuri ndani ya ligi kuu ya Zanzibar kwa misimu mingi sana kabla ya kusajiliwa klabu ya Siginda lakini baada ya mgogoro na kuamua kurudi nyumbani na kufikia klabu ya KMKM ni mshambuliaji mzuri na mtulivu ana uwezo wa kupiga vichwa hususan mipira ya  kona ni mwepesi wa kuruka sana.

Kwa saa msimu huu tunarajia kumuona ndani ya klabu ya KMKM hivyo kwa usajili wa klabu hii ya KMKM basi Chinga atakuwa kinara mkubwa ndani ya klabu yake hii mpya ya KMKM.

Salum Songoro( Mshambuliaji), moja ya wachezaji wadogo sana ndani  ya klabu ya KVZ mzuri kwenye kufunga na kumalizia mipira ya kroosi ,kimo chake ni mfupi sana ila ni mshambuluaji matata wa KVZ ndio kinara wa kufunga magoli ndani ya timu hiyo anarekodi nzuri ya kufanya vizuri kwenye kikosi cha Zanzibar Heros ila kwa bahati mbaya ya majeruhi hakuweza kuchukuliwa kwenye kikosi cha Zanzibar Heros kwa majeruhi yake.

Issa Hairdar mwalala (mlinzi) ,moja ya wachezaji vinara na tishio msimu huu ligi kuu ya Zanzibar  ndani ya klabu yake ya JKU ni mlinzi mashuhuri mwenye uwezo kuondoa hatari kwa njia zozote zile ni mtulivu katika kufanya maamuzi si mlinzi ambaye anacheza rafu sana ni mstaarabu sana.

Moja ya rekodi kubwa ni kuitwa Zanzibar Heros mara mbili mfulilizo ni chaguo namba moja la Hamidi Moroko Zanzibar Heros amecheza michezo yote kule Kenya ndio mlinzi namba moja kwa sasa ndani ya ligi kuu ya Zanzibar hakuna mbadala wake licha ya kutoitwa timu ya Taifa ya Tanzania ila huyu jamaa yuko vizuri .

Mzuri wa kupiga mipira ya juu yaani goal kick ,hata mipira ya kuunganisha alishinda magoli mawili ya aina moja ndani ya ligi kuu ya Zanzibar ya kupiga mpira wa moja kwa moja bila ya kuguswa na mtu .

Ali Humudi Balii( Mlinzi), Moja ya waziri wa ulinzi machachari ndani ya msimu huu kutoka klabu ya Mlandege msimu ulopita alituumikia klabu yake ya Miemben City pia aliwahi kuitumikia Jangombe Boys, Balii’’ hana tofauti na Issa Mwalala ila yeye hakuchukuliwa Zanzibar Heros ila ni mtulivu wakati wa kulinda mashambilizi ndani ya timu yao tunategemea kumuona akiwa kwenye ari msimu huu kutumikia vilabu tofauti kwa kila msimu wa ligi kuu ya Zanzibar .

Ibrahim Sangula (Mlinzi), moja ya walinzi matata kwenye klabu yake ya Jangombe Boys ni mchezaji mwenye heshima na anaheshimiwa kwenye klabu yake pia ni nahodha wa timu hiyo pia amebahatika kuutumikia Jangombe boys kwa muda mrefu sana.

Aliwahi kuitwa Zanzibar Heros na kuchezeshwa mlinzi wa kulia aliutendea haki namba yake hiyo na kufanya makubwa kule Kenya tunategemea kumuona akiwa kwenye kiwango chake licha ya kimo chake mfupi lakini hucheza mlinzi wa kati na kuutendea haki namba yake bila bughuza wala mapepe.

Ali Othman Mmanga (Mlinzi), yeye ni mlinzi wa kulia wa klabu ya Polisi licha ya timu yao kutokuwa na wachezaji vinara wakubwa wengi wakiwa umri wao umekwenda sana ila MManga ni moja ya walinzi hatari wa kulia wanaitetendea haki namba yake.

Rekodi yake aliitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar Heros ila na kuchezeshwa na kufanya Zanzibar kuwa ndio vinara kwenye mashindano hayo kwa mashirikiano na wenzake.

Wapo wengi sana ambao ni vinara msimu huu wa Ligi kuu ya Zanzibar hawa ni baadhi ya wachezaji ambao wanatarajia kufanya vizuri msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar ni vinara ndani ya klabu zao.