MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan Leo amezindua Mtandao wa Viongozi Wanawake Afrika Tawi la Tanzania katika hafla maalum iliyofanyika Jijini Dodoma.

Mama Samia katika uzinduzi huo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambazo zimepiga hatua katika kuwapatia Wanawake nafasi za uongozi na kufikia asilimia 36.7.

Aidha alisema jukwaa hilo linatarajiwa kuwa chachu ya kuinua takwimu zaidi za Wanawake katika Uongozi barani Afrika

Awali Mwenyekiti Mwenza wa Mtandao wa Viongozi Wanawake wa Afrika (AWLN) Tawi la Tanzania, Mary Rusimbi,amesema kuwa , umoja huo umeanza 2017 huku Tanzania ikiwa nchi ya 14 kuzindua na ulianzishwa kwa ushirikiano baina ya umoja wa mataifa na umoja Afrika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika La Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Wanawake UN Women, Hodan Addou mara baada ya kumkabidhi zawadi kwenye uzinduzi wa  Mtandao wa Viongozi wanawake Afrika Tawi la Tanzania  ambapo kauli mbiu ya Mtandao huo ni Wananwake na Uongozi Twende Pamoja Wakati ni huu uliofanyika jijini Dodoma.