Makocha 37 washiriki kwenye kozi maalum (Kozi rejea)

Jumla ya makocha 37 wameshiriki kwenye kozi maalum (Kozi rejea) kwa jiili ya kujindaa msimu mpya wa ligi mbali mbali ikiwemo ligi kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka 2018/2019 Visiwani Zanzibar.

Akifungua Mafunzo hayo Mwenyekiti wa kamati teule ya ZFA Mwalim Ali Mwalim  amewataka makocha hao kuhakikisha wanakuwa walezi wazuri wa wachezaji na vijana wadogo ili kuleta mafanikio kwenye mpira wa Zanzibar.

Aidha Mwalim Ali ameekemea na kuwaomba makocha hao kuacha tabia ya kuwapa majina makubwa wachezaji wadogo kwa kuwa hawayajengi kiufundi na kuwafanya wapotee haraka.

Kwa upande mwengine amewasa makocha hao kuwa watambue mchango wao katika kuendeleza soka la Zanzibar ikiwemo kujiongeza kielimu zaidi na wasiridhike na leseni walizinazo sasa ,ifike wakati wabadilike kimtazamo .

‘’nyinyi ni walimu lazima mkubali kuwa falsafa yenu mnaajiriwa kwa jiili ya kufukuzwa hivyo mjue lazima mtabeba lawama kubwa kwa wapenzi mkubali hizo lawama ndio kazi yenu’’ Alisema Mwalim Ali.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo kocha Abdul Ghani Musoma amesema mafunzo hayo yatajikita kwenye maaeneo ikiwemo kutaka tathimini kwa makocha hao kwa mashindano yote yanayondaliwa na ZFA.

Aidha Kocha Musoma amesema kozi hiyo pia itakuwa na semina ndogo ndogo kwa wakufunzi hao ili kuwajenga hata kuwa viongozi na wakuregenzi wa ufundi ndani ya vyama vya michezo.

‘’Mafunzo yetu yatajikita katika aina za ukufunzi za kisasa ambako dunia ipo inataka watu wawe wataalamu’’ Alimalizia Kocha Musoma.

Kozi hiyo (Refresh Coz) Kozi rejea ndo kwa mara ya kwanza inafanyika visiwa ni Zanzibar na itakuwa ya siku nne kwa jiili ya kuwaweka sawa makocha wa Zanzibar kwa jiili ya msimu ujao wa ligi mbali mbali za Zanzibar.