Makonda awatupia dongo wanaompinga Rais Magufuli adai wameshindwa hata kujenga makao makuu ya chama chao

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameeleza kushangazwa na hatua ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuonesha kumpinga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile alichokisema kuwa wanapinga maendeleo.

Makonda ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la Msingi la upanuzi wa barabara ya Kimara hadi Kibamba yenye urefu wa kilometa 19 ambapo viongozi mbalimbali walishiriki.

Makonda “hivi mkikaa na kumpinga Rais, mnampinga kwa kosa gani hasa. Hivi mnapokaa nyinyi na akili zenu timamu huwa mnawaza nini, meshindwa hata kujenga makao makuu ya chama chenu,” amesema RC Makonda.

Awali kwenye mkutano huo, Makonda aliwatambulisha viongozi hao wa upinzani akiwemo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, pamona na Mbunge wa Kibamba John Mnyika.

Niwatambue wabunge wote wa Mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mbunge Mwenyeji na wamekuja sio kwa sababu hawana pa kwenda ila kwa sababu wamebanwa vibaya.” Amesema Makonda.