Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda mekabidhi ofisi rasmi kwa Mkuu wa mkoa mpya wa DSM Aboubakar Kunenge leo na kusema kuwa Rais Magufuli bado ni Role Model wake.

“Rais aliniamini na kuamini ninachofanya ni kwa faida ya Watanzania na tukaibuka kidedea dhidi ya mapambano ya Dawa za Kulevya, JPM ni Rais msikivu kwangu tena mnyenyekevu na Mcha Mungu ambaye daima nitaendelea kumuenzi kwa vitendo” amesema Makonda 

“Hata napotoka katika ofisi hii JPM bado ni Role Model wangu, juzi mmoja Mtu nilimwambia msithubutu kumchezea Dkt.Magufuli mkafikiri Makonda hatomtetea kwasababu hayupo kwenye kiti cha U-RC, nilikuwa jeshini ninazo medali za kivita, ni Askari aliyeko Backbencher lakini mwenye uwezo mkubwa wa kupigana vita yoyote, RC, Mambosasa na Timu yenu mkihitaji uzoefu wangu katika mapambamo ya kumtetea JPM hata saa tisa usiku nitanyanyuka” Makonda