Madiwani wa Halmashauri ya Mji Masasi wamedai malipo ya Korosho kwa Wakulima ni chanzo cha ongezeko la uwepo wa kina dada wanaofanya Biashara ya Ngono

Wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wamesema, katika Wilaya yao kumekuwa na Wasichana kutoka sehemu mbalimbali nchini wanaofanya Biashara ya Ngono

Diwani wa Kata ya Mkuti, Hamza Machuma amesema Kata yake kuna makundi ya Wasichana ambao wamekodi vyumba mitaani na biashara yao kubwa ni Biashara ya Ngono

Alisema, wasichana hao mara nyingi wamekuwa wakionekana katika kipindi cha misimu ya mauzo ya zao la korosho kwa vile wanafahamu Wakulima wamepata fedha

Aidha, Mbunge wa Masasi, Rashidi Chuachua amesema kwa kasi ya Wasichana kutoka maeneo mbalimbali kwenda Masasi kwa ajili ya kufanya Biashara ya Ngono ni kubwa na lazima idhibitiwe