Mama Samia azindua rasmi Tamasha la Urithi, akimwagia sifa Kikundi cha Bagamoyo Players

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mapema leo Septemba 15, 2018 amezindua rasmi Tamasha la Urithi (Urithi Festival) katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma huku akikoshwa na kikundi cha Sanaa cha Bagamoyo Players kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kilichoweza kuonesha ufundi wa kucheza ngoma na maigizo ya jukwaani.

Katika tukio hilo, kikundi hicho cha Bagamoyo Players kimeweza kuwasilisha ujumbe mzito kwa jamii kupitia igizo maalum lililoonyesha jinsi viungo vya mti vinavyoishi kwa kutegemeana  huku wakiongozwa na  Mkufunzi  wa  Chuo hicho cha TaSUBa,  Mwalimu  Haji Maeda.

Wasanii wa Bagamoyo Players wakionyesha Igizo la mti kwenye tukio la uzinduzi wa tamasha hilo la Urithi (Urithi Festival) lililozinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais Mama Samia.

 

Wasanii wa Bagamoyo Players wakionyesha Igizo la mti kwenye tukio la uzinduzi wa tamasha hilo la Urithi (Urithi Festival) lililozinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais Mama Samia.

Mama  Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, akitoa hotuba yake jukwaani hapo alikili wazi kuwa kikunci hicho kimemfurahisha  sana kwa ujumbe wao huo wa igizo huku pia akiwapongeza washiriki wengine pamoja na wadau wote waliofanikisha tukio hilo la Urithi ambalo kwa mwaka huu ni mwaka wa kwanza kuanzishwa kwake.

Igizo hilo la kikundi cha Bagamoyo Players lilikuwa likielezea maswahiba ya Mti katika ugongano wa ama ufalakano lakini baadae wanakuja kukubaliana na kuwa kitu kimoja hii ni pamoja na Mti huo kugawanyika kwenye matawi, shina, mizizi na maua yake.

Tamasha hilo la Urithi linatarajiwa kumalizika Septemba 22, mwaka huu ambapo wiki nzima kwenye tukio hilo bidhaa mbalimbali za Utamaduni, ikiwemo vyakula, mavazi, ngoma za asili na nyama pori zitakuwa zikiuzwa na kuonyeshwa kwa lengo la kukuza na kuenzi Urithi wa Mtanzania.

Katika Tamasha hilo burudani mbali mbali za Igizo, ngoma na nyimbo za asili pia Viongozi wa Serikali na Taasisi mbali mbali walihudhuria.

Aidha Wasanii Nguli katika lugha ya kiswahili, sanaa na utamaduni walitunukiwa Tuzo, wasanii hao ni Shaaban Robert ambaye alitunukiwa Tuzo ya Nguli wa Lugha ya Kiswahili katika Uandishi ya Urithi Festival mwaka 2018 na kupokelewa na Mtoto wake Ikbali Robert, na Mzee Morris Nyunyusa ambaye alitunukiwa Tuzo ya Nguli wa Sanaa za Ngoma ya Urithi Festival kwa mwaka 2018 ambayo ilipokelewa na mjukuu wake.