Mamlaka ya uthibiti wa hali ya Hewa Zanzibar imewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kifupi cha upepo mkali uliofikia wastani wa kilomita 55 kwa saa na kuchukuwa tahadhari wao binafsi kwa kujiepusha na maeneo hatarishi ikiwemo kukaa chini ya Miti mirefu na kujiepusha na matumizi ya bahari.

Kiwango cha kawaida cha upepo ni Kilomita 20 ambapo ikifika kilomita 40 ni upepo mkubwa wakati Zanzibar kuanzia juzi Oktoba 22 Upepo ulifikia wastani wa Kilomita 55 hali iliyosababisha athari kwa baadhi ya maeneo hadi kupelekea kusitishwa kwa usafiri wa baharini.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya Hewa Zanzibar Ndugu Said Khamis wakati akizungumza na Zanzibar24 Ofisini kwake Chukwani Wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja.

Amesema hali ya upepo mkali inatazamiwa kupungua siku hadi siku kuanzia leo Oktoba 24.

Taarifa kamili angalia Video hapo chini: