Ofisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa ubingwa walioupata ni ubingwa wa mashabiki wa Simba na bila ya mashabiki basi wasingengekuwa mabingwa.

“Ubingwa huu ni kwenu Washabiki wetu kokote mlipo, nyie ndio mnalostahili pongezi za kwanza,nyie ndio Mastar wetu, kwangu binafsi naona bila nyie tusingekuwa Machampioni”

“Mmetupa ujasiri hata tulipokuwa dhaifu, mmetupa kila aina ya hamasa, nitawaomba uongozi wa klabu wafanye yafuatayo, kwa kuwa kikombe hiki ni chetu hadi kiyama, tukitoe kama zawadi kwenu.” amesema Manara

Mchezo huo wa uliochezwa Jana ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo kila timu ilikuwa ikipambana kusaka ushindi ila mwisho wa siku mbinu zikatoshana na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Simba inafikisha pointi 79 ambazo haziwezi timu yoyote kwa sasa pia unakuwa ni ubingwa wa 21 kwa Simba na wa tatu mfululizo kubeba kwa msimu huu ilianza msimu wa 2017/18,2018/19 na 2018/20.

Story by www.dimbani.co.tz