Kuimarika kwa udhibiti wa shughuli za madini na kuongezeka kwa uzalishaji miongoni mwa wazalishaji katika migodi mikuu, hususan ile ya Geita na North Mara, kumeinua mapato yatokanayo na uuzaji wa nje wa madini ya dhahabu kwa Tanzania.

Kwa mujibu wa tathmini ya uchumi ya mwezi ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi April, mapato yatokanayo ya uuzaji wa dhahabu yameongezeka kwa $100 milioni (takribani Sh223 bilioni) mwishoni mwa mwaka uliomalizika Machi, mwaka huu, ikilinganishwa na mwaka uliomalizika Machi, 2018.

Tathmini hiyo inaonyesha kuwa mapato yanayotokana na mauzo ya nje ya dhahabu yameongezeka kwa kiwango cha dola bilioni 1.68 katika mwaka uliomalizika mwezi Machi mwaka huu, kutoka dola bilioni $1.53 kiwango kilichorekodiwa wakati wa mwaka uliomalizika Machi 2018.

BoT inasema kuwa uuzaji wa bidhaa nyingine katika nchi za nje umeongezeka,

na mafanikio haya yametokana na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi katika mwaka uliomalizika Machi 2019 hadi dola bilioni $8.5 kutoka dola bilioni $8.4 katika kipindi kama hicho hicho kilichomalizika 2018.