Marekani na Urusi zimewasilisha maazimio yanayokinzana kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kisiasa nchini Venezuela.

Marekani inamtaka Rais Nicolas Maduro kukubali kufayika kwa Uchaguzi mpya wa urais haraka iwezekanavyo, lakini pia kuhusu misaada ya kibinadamu kuingia nchini humo.

Hata hivyo, Marekani haijasema inataka uchaguzi huo ufanyike lini, wakati huohuo ikiitaka Jumuiya ya Kimataifa kumuunga mkono Kiongozi wa upinzani, Juan Guido kama Kiongozi wa Venezuela.

Urusi nayo inataka katika azimio lake, mataifa ya nje yaache kuingilia siasa za ndani ya Venezuela na Rais Nicolas Maduro, atambuliwe kuwa Rais halali wa nchi hiyo.

Marekani na Urusi zinatarajiwa kutumia kura zao za veto, kuzuia maazimio hayo.