Marekani yaingilia kati sakata la Mwandishi kupotea Uturuki

Rais Donald Trump wa Marekani ameahidi kwamba ukweli wote utapatikana kuhusiana na kupotea kwa mwandishi mwenye asili ya Saudia Jamal Khashoggi ambaye kwa mara ya mwisho alikwenda katika majengo ya Ubalozi wa Saudia nchini Uturuki oktoba mbili mwaka huu.

Trump amewaambia waandishi wa habari kwamba sana jambo hilo na mamlaka za Saudia na kutaka maelezo ya kina kutolewa.

“Hatuwezi vumilia vitendo kama hivyo kutokea kwa waandishi ama kwa mtu awaye,” Trump

Ameongeza kwamba wanahitaji kila kitu kinachohusiana na kutoweka kwa mwandishi huyo

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na maofisa wa juu tayari wamefanya mazungumzo na mwana mfalme Mohammed Bin Salman hapo jana na wakahitaji maelezo zaidi juu ya tukiuo hilo.

kamera za CCTV zinazothibisha eneo ambalo linahusika moja kwa moja na upoteaji wake
Kamera za CCTV zinazothibisha eneo ambalo linahusika moja kwa moja na upoteaji wake

Hapo jana siku ya jumatano,baadhi ya vyombo vya habari vya Uturuki vilionyesha baadhi ya vipande vya picha za kamera za CCTV zinazothibisha eneo ambalo linahusika moja kwa moja na upoteaji wake.

Imebainika kuwa maafisa usalama wa Saudia wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Uturuki kupitia uwanja wa ndege wa Istanbul.

Kitu kingine kilichoonyeshwa kwenye picha hizo za video runinga ya Uturuki ya TRT zinaonyesha gari jeusi likifika eneo hilo la ubalozi na ambalo linadhaniwa kuhusiaka katika tukio hilo.

jamal

Pia utepe mwingine wa picha hizo za video unalionyesha kundi jingine la watu wanaodhaniwa ni raia wa Saudia wakiingia uwanja wa ndege wa Istanbul na ambao pia wanaonekana katika baadhi ya hotel za mjini Istanbul.