Jeshi la Marekani limekiri Ndege yake kutunguliwa na jeshi la Iran ilipokuwa kwenye anga ya kimataifa eneo la mpaka kati ya ghuba ya Oman na Uajemi, maafisa wa Marekani wameeleza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Awali vikosi vya kijeshi vya Iran vilidai kuwa vimeshambulia ndege ya kijasusi isiyo na rubani kwenye anga la Iran. Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti tukio hilo dhidi ya ndege isiyo na rubani walioiita RQ-4 Global Hawk, kusini mwa jimbo la Hormozgan.

Jeshi la Marekani awali halikuthibitisha kama ndege yake imeangushwa, huku msemaji akikana taarifa kuwa ndege ya Marekani ilikua kwenye anga la Iran.

Ndege isiyo na rubani inayodaiwa na Iran kuwa ya Marekani

Tukio hilo limetokea siku kadhaa baada ya wizara ya ulinzi ya Marekani kusema kuwa watapeleka vikosi 1,000 zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya kutokea mvutano kati ya Marekani na Iran.Shirika la Habari la Iran lilichapisha picha hii sambamba na ripoti yake

Marekani iliishutumu Iran kushambulia kwa mabomu meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Mzozo huo ulishika kasi siku ya Jumatatu wakati Iran iliposema kuwa itazidisha kiwango cha urutubishaji wa madini ya Urani kinyume cha makubaliano na mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015.

Iran imefikia uamuzi huo baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

Msemaji wa jeshi nchini Marekani awali aliiambia Reuters kuwa ”hakuna ndege iliyokuwa ikiruka kwenye anga la Iran leo” lakini hakutaka kuzungumza zaidi.

Ramani ya Iran