Marekani yatishia kuiwekea vikwazo mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC

Marekani imetishia vikwazo dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ikiwa itaendelea na mikakati yake ya kuwashtaki raia wa Marekani.

Mahakama hiyo kwa sasa inatathmini kuwafungulia mashtaka wanajeshi wa Marekani kwa madai ya kuwatesa wafungwa nchini Afghanistan.

Mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa John Bolton alisema mahakama hiyo sio halali na kuapa kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuwalinda raia wake

John Bolton amekuwa mkosoaji mkubwa wa wa mahakama hiyo lakini Jumatatu alitoa hotubaa kali mjiji Washington akilenga sehemu mbili.

Kwanza ni wakati mwendesha mashtaka Fatou Bensouda alituma ombi mwaka uliopita kwa uchunguzi kufuatia madai ya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan ukiwemo uliotendwa na wanajeshi wa Marekani.

Jambo la pili alilozungumzia Bolton ni hatua ya Palestina kuipeleka Israel kweneye mahakama ya ICC kufuatia madaia ya ukiukaji wa haki za binadamua huko Gaza na ukingo wa magharibi hatua inayotajwa na Israel kuwa ya kisiasa.

Bolton anasea hatua hiyo ya Palestina ni moja ya sababu zilizochangia utawala wa Marekani kuamua kufunga ofisi za kidiplomasia za Palestina mjini Washington.

Marekani ni kati ya nchi kadhaa ambazo hazijajiunga na mahakama ya ICC.

Mwaka uliopita nchi tatu za Afrika – Burundi, Gambia na Afrika Kusini ziliashiria nia yao ya kujitoa kwenye mahakama hiyo ya kimatafa ya uhalifu wa kivita ICC.

Mwezi Oktoba mwaka 2016, Burundi na Afrika Kusini waliandika kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelezea uamuzi wao wa kuondoka kutoka ICC.

Kutoridhika na mahakama hiyo kumetokana na hisia kuwa ICC ilikuwa inawalenga waafrika na haiheshimu siasa na uhuru wa nchi za Afrika. Kesi kumi kati ya tisa zilizo, kwenye mahakama hiyo zinahusu nchi za Afrika.