Rais wa Marekani, Joe Biden amehutubia taifa baada ya kurekodi vifo 500,000 vilivyotokana na virusi vya corona, idadi kubwa zaidi kufikiwa ulimwenguni.

” Kama taifa, hatuwezi kukubali mwisho huu mbaya. Tunapaswa kuepuka kufa ganzi kwa huzuni” alisema Biden

Rais na Makamu wa Rais , na wake zao, kisha walikaa kimya nje ya White House wakati wa tukio la kuwasha mshumaa.

Zaidi ya Wamarekani milioni 28.1 wamepata maambukizi ambayo pia ni idadi ya juu zaidi duniani.

”Leo ninawaomba Wamarekani kukumbuka. Kukumbuka wale tuliowapoteza na kuwakumbuka tuliowaacha,”

Rais Biden alisema akiwataka Wamarekani kupambana na Covid-19 kwa pamoja.

Story kwa msaada wa mtndao.