Mwili wa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Marin Hassan Marin, umezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Marin Hassan Marin amefariki Dunia asubuhi ya jana April 1, 2020, katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Wziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Mhe. Harrison Mwakiembe wakiwasili katika viwanja vya Msikiti wa Kibweni KMKM kwa ajili ya kuhudhuria msiba wa Mwandishi Mwandamizi wa TBC Marin Hassan Marin, uliofanyika leo saa Nne asubuhi na kuzikwa makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.