Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu asiyependa makuu kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa kipindi hiki, leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweza kuwakata ngebe baadhi ya mashabiki zake wanaomsema kuhusu mwili wake.

Kupitia ‘post’ yake yenye picha kama inayoonekana hapo juu, staa huyo wa filamu ameweza kuwajibu baadhi ya mashabiki zake kwenye sehemu ya komenti.

Wema Sepetu amejitahidi kujibu kama alivyoandikiwa kuhusiana na ‘post’ hiyo yenye picha kadhaa aliyoipandisha.