Baada ya aliyekuwa kocha  wa AS kigali kupigwa chini na uongozi kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi chake ameibuka na kusema kuwa yote anamuachia Mungu.

Djuma alikuwa kocha msaidizi wa Simba alisitishiwa mkataba wake akiwa na Kocha Mkuu Patrick Aussems na uongozi wa Simba ambapo aliibukia kwenye kikosi cha AS Kigali.
Akiwa na AS Kigali, Djuma amesimamia kuongoza timu hiyo kenye mechi 23 ambapo ameshinda mechi 7 na kutoa sare mechi 9 huku akipoteza saba hali iliyofanya uongozi wa AS Kigali kumpiga chini.

Djuma amesema kuwa amepokea taarifa za kuachwa kwa masikitiko makubwa ila hana namna zaidi ya kumuachia Mungu kwa kuwa yeye ndiye mpaji wa vyote.
 “Ni kwelii nimefukuzwa ila namuachia Mungu kwa kuwa yeye ni mpaji wa vyote, mapambano lazima yaendelee,” amesema Djuma.