Masoud Djuma sio wa mchezo mchezo, akabidhiwa timu

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma Irambona ambaye mwanzoni mwa mwezi huu wa October alifungashiwa virago pale msimbazi amethibitisha kuwa yeye si wa mchezo mchezo baada ya kupata shavu la kuwa kocha mkuu wa timu ya AS Kigali inayoshiriki ligi kuu nchini Rwanda.
Djuma anakuwa kocha mkuu ndani ya timu  mpya ambayo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja mara baada  ya kocha mkuu wa timu hiyo Eric Nshimiyimana kujiuzulu.
Timu nyingine ambayo ilikuwa ikihitaji saini ya Djuma baada ya  kuachana na Simba kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems ni Inter Class ya Burundi ambayo inashiriki ligi daraja la pili.