Donald Trump amemkosea heshima waziri mkuu wa Uingereza, waziri wa maswala ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt amesema. Matamshi yake yanajiri baada ya rais Trump kuimuita balozi wa Uingereza nchini Marekani Kim Darroch ‘mjinga’ kufiatia mgogoro kuhusu barua pepe zilizofichuliwa.

Kwa mujibu wa BBC. Aliendelea kumkosoa waziri mkuu Theresa May kuhusu Brexit , akisema kwamba alipuuzilia mbali ushauri wake na kwamba alifanya maamuzi yake ya ‘kipumbavu’.

Siku ya Jumapili barua pepe zilizofichuliwa zilionyesha balozi huyo aliuita utawala wa Trump usiojitambua.

Wakati huohuo mkutano kati ya waziri wa maswala ya biashara za kimataifa nchini Uingereza Liam Fox na waziri wa biashara wa Marekani na Wilbur Ross ulifutiliwa mbali siku ya Jumanne.

Bwana Hunt alijibu matamshi ya bwana Trump katika mtandao wa twitter: Marafiki huzungumza bila kufichana hivyobasi nitazungumza: Matamshi haya yanamkosea heshima na ni makosa kwa waziri mkuu wa taifa langu.

Jeremy Hunt na Borris Johnson

Wakati wa mjadala uliopeperushwa hewani moja kwa moja mgombea akiye kifua mbele kumrithi waziri mkuu Theresa May Boris Johnson aliulizwa iwapo angmwacha balozi huyo kuendelea , lakini alisema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kutekeleza lolote.

Bwana Johnson alisema ana uhusiano mzuri na Ikulu ya Whitehouse na kwamba ilikua muhimu kuwa na uhusiano mzuri na Marekani.

Muhariri wa maswala ya kisiasa wa BBC Laura Kuenssberg alisema kuwa mgogoro huo ni ukumbusho wa ulivyo uhusiano wa Marekani na Uingereza alioutaja kuwa na hila chungu nzima mbali na changamoto inayomkuba kiongozi wa Uingereza anayekabiliana na rais ambaye hupenda kuzua migogoro.

Lakini alikuwa Jeremy Hunt ambaye alionekana kuchukua tahadhari na kuzungumzia wazi na moja kwa moja na Donald Trump kuhusu swala hilo huku Boris Johnson akisema kwamba hajutii kuwa mtu wa karibu wa Ikulu ya Whitehouse.

Kufuatia matamshi ya rais Trump siku ya Jumatatu kwamba Marekani haitashirikiana tena na Sir Kim , wizara ya maswala ya kigeni nchini humo imesema kuwa itaendelea kushirikiana naya hadi pale itakapopata uongozi kutoka kwa Ikulu ya Whitehgouse ama rais Trump mwenyewe.

”Tuna uhusiano maalum sana na wa kimkakati na Uingereza ambao umekuwepo kwa muda mrefu- ni kitu kikubwa zaidi ya mtu yeyote binafsi” , wizara hiyo iliongezea.

Awali serikali ya Uingereza ilisema kuwa inamuunga mkono balozi wake.

Msemaji wa Theresa May alisema kuwa bwana Kim ni mchapa kazi , na afisa wa serikali anayeheshimiwa na kuthibitisha kuwa hakuna mpango kwa bi May na bwana Trump kuwasiliana kujadiliana kuhusu uhusiano wa mataifa hayo kufuatia ufichuzi huo wa barua pepe.

Serikali ya Uingereza pia imethibitisha kuwa Sir Kim hatohudhuria mkutano kati ya Ivanka Trump na waziri wa bisharaza za kimataifa Liam Fox mjini Washington.

Msemaji huyo alisema kuwa: hatohudhuria mkutano huo lakini anamuunga mkono Liam Fox kuhusu mambo mengine ya ziara yake.

Mapema siku ya Jumanne Bwana Trump alituma ujumbe wa twitter akisema: Balozi wa Uingereza ambaye ameletwa hapa Marekani sio mtu tunayemshabikia , ni mtu ‘mjinga sana’.

Azungumze na taifa lake na waziri mkuu Thereza May kuhusu mazungumzo yao ya Brexit yaliofeli na sio kukasirishwa na ukosoaji wangu kuhusu vile mazungumzo hayo yalivyosimamiwa vibaya.

Nilimwambia @ Theresa _ May jinsi ya kufanya makubaliano hayo , lakini alifanya uamuzi wake wa ‘kipumbavu’ na alishindwa . Janga.

Simjui balozi huyo lakini nimeambiwa kwamba ni mpumbavu . Mwambieni Marekani ina uchumi bora zaidi na jeshi bora duniani kwa umbali na tunazidi kuimarika kwa ukubwa na uthabiti…Ahsante Bwana rais.

Serikali ya Uingereza awali ilitaja ufichuzi huo kama bahati ambaya na imeanza uchunguzi ramsi . Ilisema kuwa Uingereza na Marekani bado zina uhusiano maalum na wa kudumu.

Barua pepe za siri kutoka kwa balozi huyo wa Uingereza zilikuwa na msururu wa ukosoaji wa utawala wa rais Trump na kusema kuwa Ikulu ya Whitehouse ilikuwa haina utendakazi wa haja na kwamba kulikuwa na mgawanyiko mkubwa chini ya uongozi wake.

Sir Kim ambaye alikuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani Januari 2016 mwaka mmoja kabla ya rais Trump kushika madaraka pia alihoji iwapo Ikulu ya Whitehouse itawahi kupata mtenda kazi , lakini pia ilionya kuwa rais huyo wa Marekani hafai kupuuziliwa mbali.

Barua hizo za 2017 zilisema kuwa uvumi kuhusu mapingano na ghasia katika Ikulu ya Whitehouse yalikua ya ukweli na kwamba sera kama swala nyeti la Iran lilizua tofauti zisizo za kawaida.By Ally Juma.