Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w) yatasomwa siku ya jumaapili tarehe 18 oktoba, 2020, siku ya jumatatu tarehe 19 oktoba, 2020 itakuwa siku ya mapumziko. siku ya alhamisi tarehe 29 oktoba, 2020 ambayo hapo awali ilipangwa kuwa siku ya mapumziko, siku hiyo sasa itakuwa siku ya kazi kama kawaida.