Jumla ya wachezaji 30 wanatarajia kuanza mazoezi ya Timu ya Taifa ya Vijana U 18 ya wanawake  upande wa Zanzibar. Mashindano hayo ni ya mpira wa mikono yatakayowakilisha kwa upande wa Tanzania na kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki na kati nchini Rwanda.

Akizugumza na Zanzibar24 kocha mkuu wa timu Kombo Ali Kombo amesema timu hiyo iliotangazwa tangu mwezi wa10 itajumuisha wachezaji kutoka maskuli mbali mbali na vikosi vya Smz ili kufanya mchujo wa kutafuta timu mmoja ya Taifa.

Aidha Kombo amesema timu hiyo inatarajia kufanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Jeshini Nyuki kwa lengo la kuwapa uzoefu kwa vile baadhi ya wachezaji wengi ni mara ya kwanza kuitwa kwenye timu hiyo ya Taifa ya Tanzania na kucheza mashindano ya kimataifa.

‘’Timu inabaraka zote za ZAHA na TAHA kwa vile tunagawana mashindano ya kimataifa sasa ni zamu ya kundaa timu ya Zanzibar hivyo tutafanya vizuri na tuko tayari kiushindani’’ Alisema Kombo Ali.

Aidha amesema mafanikio ya mchezo huo visiwani Zanzibar yanatokana na Clinic tofauti za Vijana zinazondaliwa na ZAHA kwenye mpango wake kazi wa kila baada ya miezi mitatu kufanya Clinic za mpira wa mikono ili kuinua mchezo huo ngazi ya Vijana.