Kiongozi wa zamani wa waasi wa Congo amehukimiwa kifungo cha miaka 30 jela la Mahakama ya Kimataifa ya jinai kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu .

Waoiiganaji waliomtii Bosco Ntaganda walitekeleza mauaji ya ukatili dhidi ya raia, Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), walisema mwezi Julai.

Ntaganda, ambaye alipewa jina la bandia “Terminator”, alipatikana na makosa 18 mkiwemo ubakaji, utumwa wa ngono , na kuwatumikisha watoto kama wanajeshi.

Hukumu dhidi yake ni ya muda mrefu kuwahi kutolewa katika historia ya mahakama ya ICC

Ntaganda alikuwa ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia ya utumwa wa ngono na mahakama ya ICC kwa kwa ujumla ni mtu wa nne ambaye mahakama hiyo imempata na hatia tangu ilipoundwa mwaka 2002.

Ntaganda amnbaye alizaliwa nchini Rwanda mwenye umri wa miaka 46-muasi wa zamani amekuwa akihusika na mizozo mbali mbali ya kivita nchini Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Wachambuzi wanasema kujisalimisha kwake katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda kilikuwa ni kitendo cha kujilinda kutokana na hatari iliyokuwa inamkabilibaada ya kupoteza mamlaka ndani ya kikundi chake cha waasi wa M23